1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages

 
 
 

 

 | 02.12.2008 | 03:00 UTC

Mpango wa kuidhinisha euro bilioni 200 wapingwa na matiafa ya EU

BRUSSELS


Mawaziri wa Fedha kutoka mataifa 15 ya bara la Ulaya yanayotumia sarafu ya euro wameshindwa kuafikiana kuhusu hatua ya kuidhinisha matumizi ya euro bilioni 200 kwa lengo la kuufufua uchumi.Hata hivyo wamekubaliana kuwa wanahitaji kuwa na mpango maalum utakaopambana na uchumi unaodorora.

Wiki iliyopita Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ilipendekeza hatua ya kuimarisha uwekezaji wa umma pamoja na viwango vya ununuzi kote barani Ulaya vilevile hatua ya kufutilia mbali kodi ya mauzo VAT.Kamisheni hiyo inataraji kuungwa mkono na mataifa wanachama katika kikao kitakachofanyika mjini Brussels,Ubelgiji ifikapo tarehe 11-12 mwezi huu.

Ujerumani inapinga vikali hatua ya kuchangia fedha zaidi na kusisitiza kuwa kila nchi sharti ipange bajeti zake bila shinikizo.  

 

  

  



 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Journal (english) - With Business