1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages

 
 
 

 

 | 02.12.2008 | 03:00 UTC

India yailaumu Pakistan rasmi kufuatia mashambulio ya Mumbai

MUMBAI


Wizara ya mambo ya nje nchini India imeitaka nchi jirani ya Pakistan kuchukua hatua kali dhidi ya washukiwa wa mashambulio ya bomu yaliyotokea mjini Mumbai wiki iliyopita.Marekani kwa upande wake inaishinikiza Pakistan kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa mashambulizi hayo unaoendelea.Jumla ya zaidi ya watu 170 walipoteza maisha yao na wengine yapata 300 kujeruhiwa katika mashambulio hayo yaliyotokea kwenye eneo la kibiashara la Mumbai lililojumuisha hoteli mbili za kifahari za Taj Mahal na Trident/Oberoi pamoja na kituo kimoja cha Wayahudi. India imetoa lalamiko rasmi kwa nchi ya Pakistan. Kulingana na taarifa mpya wahusika hao ni raia nchi ya Pakistan.Waziri mkuu wa Pakistan Yousef Raza Gilani anasisitiza kuwa nchi yake itawajibika.


GO TO AUDIO

GILANI CLIP

Pakistan itatimiza wajibu wake na tumewaomba wandani wetu wote kutumia uwezo wao kuingilia kati ili kusawazisha mambo.Nadhani mambo yatakuwa mazuri kwani baadhi ya maafisa wa ujasusi wamechukua dhamana ya makosa ya kijasusi yaliyotokea.


Wanajeshi wanaripotiwa kumalizia shughuli ya kuondoa maiti kwenye hoteli ya  kifahari ya Taj Mahal.Afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa India amejiuzulu kwa sasa na wengine kuwasilisha nyaraka za kujizulu.





 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Europa Aktuell - Das Magazin aus Brüssel