Matukio ya Kisiasa | 09.10.2008
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yailaumu Rwanda kwa jeshi lake kuunga mkono wapiganaji wa CNDP wa Laurent Nkunda
Jeshi la DRC linahakikisha uungwaji mkono wa wanajeshi wa Rwanda kwa wapiganaji wa CNDP wa Laurent Nkunda.
Kwa upande wake serikali ya Kongo imeomba Baraza la Usalama la umoja wa mataifa liitahadharishe Rwanda kutokana na uvamizi wa ardhi yake na wanajeshi wa nchi hiyo.MONUC imetoa mwito wa usitishwaji mapigano kwenye mtaa wa Rutshuru.
Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.













